24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mwili wa Wakili Nimrod Mkono kuwasili Alfajiri ya Mei 27

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwili wa aliyekuwa mbunge wa Musoma Vijijini na baadaye mbunge wa Butiama mkoani Mara, Wakili Nimrod Mkono unatarajiwa kuwasili nchini alfajiri ya Mei 27, mwaka huu ukitokana nchini Marekani.

Taarifa iliyotolewa leo Mei 19, 2023 na Kamati ya Kuratibu Mazishi ya Wakili Mkono imeeleza kuwa: “Kamati ya Kuratibu Mazishi ya Wakili Nimrod Mkono, inapenda kutoa taarifa rasmi kwa umma kuwa mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nchini alfariji ya Mei 27, 2023.

“Mwili utapokewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kupelekwa nyumbani kwake Masaki,” imeeleza taarifa hiyo ya kamati.

Aidha, imeongeza kuwa mazishi ya Wakili huyo yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwake kijijini Kigori.

“Mazishi ya Wakili Mkono yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwake Kijijini Kigori, Busegwe, Wilaya ya Butiama mkoani Mara. Ratiba kamili ya shughuli yote ya kupokea, kuaga hadi kusafirisha mwili kwenda Kigori itatolewa baadaye.

“Familia inawashukuru ndugu, jamaa, marafiki, na Serikali kwa kuwa pamoja nayo kwa muda wote huu mgumu wa msiba. Kamati inaomba ndugu, jamaa, na marafiki waendelee kushirikiana na familia kwa hali na mali ili kuupokea mwili na baadaye kuupumzisha,” imeeleza taarifa hiyo.

Wakili Mkono alifariki dunia Aprili 18, mwaka huu wakati akipatiwa matibabu nchini Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles