26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Nasty C awaonjesha mashabiki ladha ya ‘Black And White’

NA MWANDISHI WETU

STAA wa muziki wa Hip Hop kutoka Afrika Kusini, Nsikayesizwe Ngcobo ‘Nasty C’ amechia vipande vya video vinavyopatikana katika wimbo wake wa Black and White.

Video ya wimbo huo ambao umeongozwa na director mkali Kyle white amemshikirisha Ari Lenox.

Kuachiwa kwa video hiyo kumeamsha hisia za wengi hasa kutokana na wimbo kuwa wa kimapenzi huku ukiawagusa wengi baada ya Shamrashamra za Valentine’s Day.

Video ya ngoma hiyo imechukuliwa katika maeneo tofauti tofauti ya Majiji ya Cape Town, Afrika Kusini na Washington DC, Marekani.

Muda mchache baada ya albamu ya tatu ya Nasty C iitwayo ZULU WITH SOME POWER, mashabiki wa mwanamuziki huyo mwenye tuzo kibao, wamesema wimbo wa Black and White ni kati ya kolabo bora zinazopatikana kwenye albamu hiyo.

Mwanamuziki huyo ambaye ndiye anayeongoza nyimbo zake kuwa kusikilizwa zaidi mtansaoni (streamed) nchini Afrika Kusini ameendelea kuwa kipenzi cha wengi kutokana na nyimbo zake kujaa utofauti wa kitamaduni na kimuundo.

Wimbo huo ni miongoni mwa soundtrack (Rhymes of Zamunda) kwenye filamu inayosubiriwa kwa hamu, Coming 2 America.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles