28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Namungo yaula tena mkataba mnono na SportPesa

NA MWANDISHI WETU

WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Namungo, wataendelea tena kunufaika na mkataba mnono kutoka SportPesa baada ya kampuni hiyo ya michezo na burudani kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Huu utakuwa ni mjumiusho wa miaka miwili tangu kumalizika kwa mkataba wa kwanza na klabu hiyo kutoka Ruangwa mkoani Lindi.

Akizungumza kwa niaba ya klabu, Mwenyekiti Hassan Zidadu aliwashukuru SportPesa kwa kuendeleza mkataba na wao kwa mwaka mwingine tena akisisitiza hii ni ishara ya Namungo kukubalika na damira yao ya kuboresha uendeshaji wa klabu.

“Kama klabu tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu kwa kufanya vizuri maana nyinyi ni kama wawekezaji mkiwa na nia kubwa ya kuhakikisha klabu inajiendesha na kufikia malengo yake,” alisema.

Zidadu alithubutu kusema bila SportPesa wasingefika hatua ya 16 bora kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa, Tarimba Abbas, alianza kwa kuwapongeza Namungo kwa kujiendesha vizuri na kuhakikisha timu inafanya vizuri barani Afrika na kuipa si Tanzania sifa nzuri bali hata SportPesa.

“Hii ndio sababu iliyotufanya kuendelea kuwadhamini Namungo, ukiiangalia vizuri klabu ya Namungo tangu ianze mpaka sasa unaweza kuona ni jinsi gani ilivyo na moyo wa kujituma na kuhakikisha wanafika mbali,” alisema.

Tarimba alisema SportPesa inawatakia kila la kheri katika mechi zinazoendelea akiongeza kwenye mkataba waliyoingia na Namungo kuna zawadi ambazo watawapa endapo timu itafanya vizuri katika hatua za roba fainali, nusu fainali na hata kuchukua ubingwa.

SportPesa ni wadhamini wakuu wa klabu za Yanga na Simba na kwa sasa wameongeza mkataba wa mwaka mmoja kwa klabu ya Namungo ambayo nayo inashirika Ligi Kuu Tanzania Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles