24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

NASA YAPANGA KUMWAPISHA RAILA URAIS

NAIROBI, KENYA

MUUNGANO wa upinzani wa NASA umesema unaendelea na mpango ya kumwapisha kinara wake Raila Odinga kuwa rais iwapo Rais Uhuru Kenyatta ataapishwa kuongoza kwa muhula wa pili.

Mkurugenzi wa muungano huo Norman Magaya alisema kumwapisha Odinga ni miongoni mwa mikakati ya NASA inayoendelea kufanyiwa kazi.

“Tuna mbinu nyingi na suala la kumwapisha Odinga ni moja ya ajenda zilizojadiliwa kwa kina. Uamuzi wa kufanya hivyo ukifikiwa umma utaarifiwa,” Magaya alisema wakati akihojiwa wakati akihojiwa na kituo cha runinga, KTN juzi jioni.

NASA imesema haitamtambua Kenyatta kama Rais ikisisitiza uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 ambao alishinda haukuwa halali.

Mahakama ya Juu ilitupilia mbali kesi mbili za kupinga ushindi wake na kushikilia kuwa alichaguliwa kihalali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles