26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Nandy na Koffi Olomide kuimba leo leo Mlimani City

Na Bright Masaki, Dar es Salaam

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Faustina Mfinanga, ‘Nandy’ leo Februari 11, 2021 ameachia Kolabo yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa burudani nchini aliyomshirikisha Mkongwe kutoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Koffi Olomide, iitwayo “Leo Leo”

Nandy amesema anafurahia kufanyakazi na Koffi kwa kuwa anaamini kazi yake itaenda mbali zaidi kwa kuwa ni msanii mkubwa.

“Kwa Mara ya kwanza tutaimba wimbo wa Leo Leo siku ya Februari 13, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam nikiwa na Koffi Olomide tutakuwa mubashara, watu wajitokeze kwa wingi,” amesema Nandy

Kolabo hiyo kubwa ya Kimataifa, itakua ya kwanza kwa Nandy kufanya na Msanii kutoka Congo na ya pili Kimataifa baada ya “Do Me” aliyomshirikisha, JoeBoy, kutoka Nigeria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles