31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Ay kucheza filamu na Robert David wa Hollywood

Na Bright Masaki, Dar es Salaam

Mkali wa Hip hope nchini, Ambwene Yessaya, Maarufu ‘AY’ amefunguka kuwa safari yake ya hivi karibuni nchini Marekani ni kwa ajili ya kwenda kutengeneza Filamu.

AY amesema kuwa kati ya Nyota watakao kuwemo kwenye Filamu hiyo ni pamoja na ni pamoja na wakongwe wa Kiwanda cha Filamu Marekani, Holly Wood, akiwemo, Robert Davi.

“Mungu ni mkubwa katika kila njia kutoka Tanzania hadi Marekani, (GOD IS GREAT All the way from Tanzania to Hollywood / Las Vegas to make a FILM with the Living Legend Actor/Musician” ameandika AY kupitia ukurasa wake wa Instagram kwenye posti akiwa na nguli huyo wa filamu na muziki, Robert Davi.

Robert Davi ambaye mkongwe kwenye ulimwengu wa filamu miongoni mwa filamu maarufu alizocheza ni pamoja na The Butcher, Predator 2, Expendables 3 na nyingine nyingi.

AY pia sio mgeni kwenye tasnia hiyo kwani alishacheza filamu kama “Girlfriend” iliyokuwa imesheheni mastaa kama TID, Monalisa, Jay Moe, GK na wengine wengi iliyotoka mwaka 2003.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles