28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

AliKiba kuanza rasmi kutumia akaunti yake YouTube

Na Bright Masaki, Dar es Salaam

Nyota wa muziki nchini, Ali Saleh Kiba maarufu Ali Kiba au King Kiba, ameweka wazi kuanza kuitumia upya akaunti (chaneli) yake ya YouTube iitwayo “AliKiba” ambayo alikuwa ameacha kuitumia kwa takribani miaka miwiwli

AliKiba ambaye anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake wa “infidèle” ambao ndani amaeimba baadhi ya mashairi kwa lugha ya kifaransa ameyasema hayo wakati akizungumza na MtanzaniaDigital Februari 11, 2021.

“Chaneli yangu ya Youtube yenye jina ‘AliKiba’ imerudi nawaomba mashabiki zangu wa subscribe, pia na kuwakumbusha album yangu inakuja,” amesema Alikiba.

Ikumbukwe, kwa kipindi cha Mwaka mmoja na miezi 10, AliKiba alikuwa akitumia chaneli ya King’s Music Records kuweka video zake kuanzia wimbo “Mshumaa”, “Dodo”, “So Hot”, “Mediocre” na “Infidèle”.

AliKiba ambaye kwasasa yupo nchini Nigeria, video yake ya mwisho kupandishwa kwenye chaneli yake ya mwanzo ‘AliKiba’ ilikuwa ni MBIO, ilipandishwa April 26, 2019, hadi sasa inazaidi ya Views milioni 124.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles