28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Jay Dee kuachia albamu yake ya 20

Na Bright Masaki, Dar es Salaam

Msanii Mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura, ‘Lady Jay Dee’, anatarajia kuachia albamu yake ya 20 kesho Februari 12, mwaka huu katika ukumbi wa Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Februari 11, Dar es Salaam, Jay Dee amesema kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo tofauti tofauti zikiwemo zile zinazohusu mapenzi.

“Katika albamu yangu nyimbo zinazojulikana ni mbili tu, lakini zingine zote ni nyimbo mpya, nimeweza kushirikiana na muandaaji wa muziki, Man Walter.

“Hivyo nimejiandaa kutoa burudani nzuri kwa mashabiki wangu katika kutambulisha albamu yangu ya 20, hivyo hakuna atakayejuta kuja kwenye uzinduzi huu,” amesema Jay Dee.

Kuhusu mahusiano yake Malkia huyo wa Bongo Fleva amesema kwa sasa hayupo tayari kuzungumzia mahusiano yake na mpenzi wake kama yupo au hayupo na kwamba jambo la msingi ni mashabiki wajitokeze kesho ili watapate kumfahamu mpenzi wake huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles