Nana wa Diamond wamdatisha Swizz Beatz

0
743

Diamondss-2NA CHRISTOPHER MSEKENA

RAPA na prodyuza wa muziki duniani, Kasseem Dean maarufu kwa jina la Swizz Beat, ameonekana kuvutiwa na nyimbo mbili za msanii, Diamond Platnumz.

Staa huyo anayeishi Marekani ameweka vipande vya video katika kurasa zake za mitandao ya kijamii ikimuonyesha akisikiliza na kucheza nyimbo za Diamond ‘Nataka Kulewa’ na ‘Nana’ huku akiandika ujumbe kwamba anafurahia midundo ya Afrika.

Hii siyo mara ya kwanza kwa prodyuza huyo wa muziki kusikiliza nyimbo za Afrika, ameshaonekana akisikiliza na kucheza wimbo wa msanii wa Nigeria, Wizkid huku ujumbe wake ukiwa ni kwamba anapenda midundo ya Afrika ndiyo maana anasikiliza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here