MWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amesema hupendelea uhusiano wa kimapenzi na wanaume wenye umri mkubwa kwake ili aweze kujifunza mengi kutoka kwao hata kama hawatokuwa wote maisha yote.
Lulu alisema kipindi alipokuwa katika uhusiano na wanaume wakubwa, alijifunza mambo mengi ambayo yanaendelea kumuweka daraja la juu katika mafanikio ya maisha yake ya sasa.
“Kipindi chote ambacho nimejikita kwenye uhusiano wa kimapenzi, nilikuwa nikipenda kuwa na watu wazima kwa kuwa naamini wanabadilisha maisha yangu kwa kuachana na maisha ya starehe kila kukicha kama wafanyavyo wanaume vijana.
“Nikisema niwe na desturi ya kutembea na vijana, lazima tutaendekeza starehe ambazo mwisho wake utakuwa mbaya katika maisha,” aliweka wazi Lulu.