26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Shein aahidi kuipaisha zaidi Zanzibar

2dk-sheinNa Mwandishi Wetu, Zanzibar

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Mohammed Shein, amesema amedhamiria kuipaisha Zanzibar kwa kuwa uwezo huo anao.

Amesema kwamba, pamoja na majukumu mengi aliyonayo, kazi hiyo ataifanya katika miaka mitano ijayo kama atafanikiwa kuendelea kukiongoza kisiwa hicho.

Kutokana na hali hiyo, amewatahadharisha Wazanzibari wasiwachague wagombea waongo ambao mara zote wamekuwa wakisema uongo majukwani kwa lengo la kupata madaraka.

Dk. Shein ambaye anatetea nafasi yake ya urais wa Zanzibar, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi katika uwanja wa Galagala uliopo Mjini Magharibi, Unguja.

“Kwa kweli bado nina nia ya kweli dhati ya kuwatumikia Wazanzibari kwa sababu uwezo huo bado ninao. Nawaomba sana vijana msidaganywe na wanasiasa wasiokuwa waaminifu kwani hakuna rais atakayekuja kutoa ajira kwa kila mzanzibari kwani hilo nimeliona baada ya kuizunguka dunia hii.

“Kwa kuwa bado nina uwezo, nimelazimika kuja na mambo mbalimbali yatakayoipaisha Zanzibar kiuchumi ikiwamo ujenzi wa kiwanda cha samaki, uwekezaji katika sekta ya uvuvi na ujenzi wa kiwanda cha maziwa.

“Yote hayo ni mambo ya msingi kwa sababu yatasaidia kuzalisha ajira na pia yatawawezesha wananchi kuweza kukabiliana na gharama za maisha,” alisema.

Katika kuhakikisha Zanzibar inasonga mbele kiuchumi, Dk. Shein alisema Serikali yake hivi karibuni itazindua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume utakaokuwa chachu ya maendeleo kisiwani humo.

Kuhusu suala la wazee, alisema kuanzia mwakani, kila mzee aliyefikisha umri wa miaka 70, atakuwa akipewa pesheni ya Sh 20,000 kila mwezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles