24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Namungo FC, SportPesa damdam

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

NAMUNGO FC yenye maskani yake Ruangwa, Lindi inayoshiriki Ligi Kuu Bara inazidi kuoga noti baada ya kuogezewa mkataba wa mwaka moja wa udhamini kutoka kampuni ya michezo na burudani ya SportPesa Tanzania.

SportPesa imeingia makubaliano hayo ya kuendelea kuidhamini Namungo FC baada ya pande zote mbili kufikia muafaka mzuri.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa SportPesa, Tarimba Abbas, alisema wana furaha kubwa kufikia makubaliano mazuri ya kuendelea kuidhamini Namungo FC.

Tarimba alisema kuwa mkataba wa mwaka mmoja wameingia na Namungo FC baada ya ule wa awali ukitarajiwa kumalizika mapema Januari 2022.

“Tunafuraha kubwa kufikia makubaliano mazuri na Namungo FC baada ya kufanya mazungumzo yaliyotushawishi kuendelea kutoa udhamini, tunaamini kupitia udhamini huu utasaidia katika masuala ya maendeleo ya Namungo FC.

“Kama SportPesa tutaendelea kuunga mkono mchezo wa soka kwa kupitia udhamini ambao tunaoutoa kutoka katika klabu mbalimbali zikiwemo klabu kubwa za Simba na Yanga,” alisema Tarimba.

Naye Mtendaji Mkuu wa Namungo FC, Omary Kaya, aliishukuru SportPesa kwa udhamini ambayo wamekuwa wakiwapatia.

“Hivyo tutaendelea kufanya kazi pamoja na SportPesa kwa kutimiza masharti ya kimkataba ikiwemo kuwatangaza vizuri na pia nichukue nafasi hii kuwapongeza SportPesa kwa juhudi kubwa wanazoendelea katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha mchezo wa soka unapiga hatua kupitia udhamini wanaoutoa,” alisema Kaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles