27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Karagwe yakamilisha madarasa 80 ya elimu Msingi na Sekondari kwa asilimia 95

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digita

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Karagwe amewapongeza viongozi wa Chama na Serikali wilayani Karagwe kwa usimamizi dhabiti wa fedha za maendeleo ya elimu Msingi na Sekondari kiasi cha Sh bilioni 1.7 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kupitia mpango wa Uviko-19.

Pongezi za Waziri Bashungwa zinafuatia kukamilika kwa ujenzi wa vyumba 80 vya madarasa kwa zaidi ya asilimia 95 katika wilaya hiyo kabla ya kuanza kwa mhura mpya wa masomo kwa mwaka 2022.

Akiwa jimboni kwake Karagwe katika kata ya Chonyonyo waziri Bashungwa ameelezea furaha yake kuona matokeo chanya yaliyotarajiwa yakitimia kwa wakati kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya viongozi wa ngazi za shina, vijiji, kata hadi wilaya pamoja na wananchi kwa ujumla wao.

Waziri Bashungwa pia ameitumia fursa hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais Samia kwa fedha nyingi za maendeleo ambazo serikali yake imezitoa kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu mbalimbali katika wilaya ya Karagwe ikiwa ni pamoja na miradi ya barabara, maji, afya pamoja na mikopo ya vijana na wanawake.

Akizungumzia maboresho katika zao la kahawa, Waziri Bashungwa amesema licha ya Serikali kuimarisha ushirika lakini pia imeruhusu wanunuzi binafsi ili kuongeza ushindani wa bei, na hamasa kwa wakulima kuendelea kulima zao la kahawa kutokana na mafanikio ya moja kwa moja wanayoyapata.

Akiwa jimboni Karagwe, Waziri Bashungwa amezitembelea kata za Igurwa, Nyakabanga na Chonyonyo na kukutana na Viongozi wa Mashina yaani mabalozi, Viongozi wa matawi na kata wa Chama Tawala CCM, pamoja na watumishi wa Serikali ngazi za vijiji na kusikiliza maoni na matamanio yao pamoja na kuwatakia heri ya sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles