25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mechi za mwisho za kufunga mwaka 2021, NPL na EPL

Huku mwaka 2021 ukibakiza saa kadhaa kufika ukingoni, kuna mechi tatu zimesalia kukamilisha raundi ya 11 ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ambazo zitachezwa mwisho mwa mwaka na mwaka mpya.

Aidha, kuna mechi moja ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyosalia kwa mwaka huu, kabla ya mechi nyingi za EPL zitakazochezwa siku ya Mwaka Mpya.

Baada ya michezo hiyo ligi zote mbili zitaenda kwa mapumziko madogo kabla ya kuendelea Januari 14, 2021, Numugo FC iliyo nafasi ya nane na points 13 iliwakaribisha Biashara United Mara walio katika nafasi ya 15 kwenye jedwali mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Mchezo wa kufunga mwaka leo Ijumaa Desemba 31, 2021 utawakutanisha vinara Young Africans wataomenyana na Dodoma Jiji FC katika uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam saa 1 usiku.

Kama ilivyozoeleka Wanachiambao wanaongoza ligi wakiwa na points 26, watataka kujiandikishia ushindi wa mapema dhidi ya miamba hiyo ya Dodoma inayoshika nafasi ya 6 ikiwa na points 16, ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi dhidi ya Mabingwa wa sasa, Simba SC ambao watacheza na Azam siku ya mwaka mpya.

Simba SC ambao wana mchezo mkononi dhidi ya Kagera Sugar pia wako katika hali nzuri zaidi ya kucheza na watajaribu kuendelea kutumia presha na kuanza mwaka kwa matumaini.

Hivyo timu zote zinajua huu ni mchezo muhimu kushinda ikiwa wanataka kwenda sambamba na Wananchi kwenye mbio za kuwania ubingwa.

Betway inatoa uwezekano mkubwa wa kamari wa kandanda kwenye mechi zijazo za ndani na kimataifa katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka wa 2022, kwa alama nzuri na za kijanja, tembelea soccer betting.

Programu ya Betway ni rahisi kupakua na inaoana na vifaa vya IOS na Andriod ili kurahisisha kamari popote ulipo mjini na vijijini.

Manchester United imekamilisha mwaka 2021 kwa kuitandika Burnley bao 3-1 usiku wa kuamkia leo pale Old Trafford.

Manchester United wameendeleza rekodi yao ya kutokufungwa chini ya Kocha Ralph Ragnick, hivyo licha ya wachezaji wake kuonekana kukabiliwa na hali mbaya kwa siku za karibuni lakini haikuwa sababu ya wao kushindwa kuiadhibu Burnley.

Burnley kwa upande mwingine bado inaendelea kukabiliwa na jinamizi la kutaka kushuka daraja msimu huu kutokana na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha.

Siku ya mwaka mpya itafunguliwa kwa pambano litakalokutanisha miamba iliyo ndani ya ToP Four ya EPL ambapo Arsenal itacheza na Manchester City.

City inaongoza kwa pointi 8 na imekuwa katika hali nzuri ya kufunga mabao. Upande wa Arsenal, ambayo Kocha wake Mikel Arteta atakosa mechi hii lakini wanatarajia kuendeleza mfululizo wao wa ushindi na kupunguza mapumziko ya City kileleni mwa msimamo.

Michezo mingine itakayofanyika siku ya kwanza ya mwaka mpya ni Leicster vs Norwich, Watford vs Tottenham Hotspur na Crystal Palace watawakaribisha West Ham United katika mchezo wa mwisho kwa jumamosi.

Jumapili tena inawakutanisha miamba mingine miwili ambayo kila mmoja nawania ubingwa katika mechi ya Chelsea dhidi ya Liverpool, timu zote mbili zitakuwa na matumaini kuwa Arsenal itaisimamisha Man City.

Hata hivyo, Chelsea itawakosa baadhi ya nyota wake kutokana na kukabiliwa na majeruhi, hivyo itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Liverpool.

Ingawa timu zote mbili hazikupata matokeo ya kuridhisha kwenye michezo ya awali kwani Liverpool ikipoteza kwa Leicster City na Chelsea kutoka sare na Brighton.

Michezo mingine itakayofchezwa Jumapili ni Brentford vs Villa, Everton vs Brighton, Leed vs Burnley na Southampton vs Newcastle.

Newcastle wanatarajia kupata matokeo chanya kutokana na uchezaji wao bora walipotoka sare dhidi ya Manchester United katika mechi yao ya mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles