25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

NAMNA YA KUJIBU MASWALI UNAYOULIZWA KWENYE USAHILI

Na JOSEPH LINO


USAILI wa ajira (job interviews) husababisha hofu na msongo wa mawazo kwa vijana wengi kabla au baada ya kutoka chumba cha usaili.

Tatizo hilo hutokana na hofu inayojenga wakati wa kujibu maswali unayoulizwa  na watu ambao wamekuzunguka wakati wa kufanyiwa usaili.

Wanataaluma vijana ambao kwa mara ya kwanza wanaitwa kwenye usaili wa ajira hushindwa kujieleza au kujibu maswali ipasavyo, yanayoulizwa kwa msingi wa kutaka kujua uwezo wako kwa namna moja au nyingine.

Kujibu maswali ya usaili hakuhitaji ‘mbwembwe’ nyingi – kuwa mjuaji au maelezo, isipokuwa waajiri huhitaji majibu ya wazi na mafupi yenye mvuto, ambayo hayaleti maswali mengine kwa mwaajiri.

Wataalamu wa ajira walijaribu kuangalia baadhi ya maswali ambayo ukifanikiwa kujibu kama ipasavyo, utakuwa kwenye nafasi kubwa ya kumshawishi mwajiri kukupa nafasi moja kwa moja.

Hii ni baadhi ya mifano ya maswali na majibu yenye ushawishi mkubwa kwa mwajiri, ambayo ukiweza kuyajibu kwa kujiamini utapata ajira bila kutoka jasho la hofu.

 

SWALI: Kwanini upewe ajira kwetu?

JIBU: Kama mkiniajiri, itakuwa fursa yangu kubwa kuonesha ujuzi wangu. Kila lengo nililoweka nitahakikisha nalikamilisha ndani ya wakati wake.

 

SWALI: Elezea sababu zilizokufanya uache kazi yako ya awali

 

JIBU: Kwa sababu ya kuboresha na kuongeza ujuzi, pia natafuta fursa bora zaidi.

 

SWALI: Kwanini umekaa muda mrefu bila kupata ajira?

 

JIBU: Nilikuwa najiendeleza katika taaluma yangu

SWALI: Tuambie uwezo wako wa kufanyaka kazi katika mazingira ya kusukumwa na kusimamiwa

 

JIBU: Huwa najiweka katika mazingira ya kutulia na kuweka akili yangu katika majukumu niliyopewa nikiwa mtulivu.

 

SWALI: Unamatarajio gani kutoka kwenye ajira hii?

 

JIBU: Kuboresha na kuendeleza taaluma yangu ili niwe na maisha bora ya baadae.

 

SWALI: Eleza namna unavyoweza kujisimamia mwenyewe

 

JIBU: Nitakuwa nafanya kazi niliyopewa nikishirkiana na wasimamizi wangu na viongozi juu ya namna ya kumaliza kazi kabla ya muda uliopangwa.

 

SWALI: Je, wewe ni mchapakazi?

 

JIBU: Ndio, mchapakazi ambaye katika ajira yangu ya awali nilikuwa miongoni mwa watu waliofanikisha miradi kabla ya muda uliopangwa.

 

SWALI: Kitu gani kinakukera miongoni mwa wafanyakazi wenzako?

 

JIBU: Naamini katika kufanya kazi kwa pamoja. Hata kama nikikerwa na kitu chochote, huwa najaribu kuepuka isipokuwa kama ni kitu cha binafsi.

SWALI: Unategemea kufanya kazi kwa muda gani kama ukipewa ajira?

 

JIBU: Kwa muda mrefu kama nitaendelea kuongeza kitu katika taaluma yangu.

 

SWALI: Je, mwenyewe unajiona kufanikiwa?

 

JIBU: Ndio, ukiachana na uwezo wa taaluma yangu, nadhani nimepata watu sahihi wa kufanya nao kazi.

 

SWALI: Unajiweka nafasi ipi katika miaka mitano ijayo?

 

JIBU: Najiona mwenyewe katika nafasi ya juu huku nikiongoza miradi mikubwa ya kampuni hii.

 

SWALI: Uwezo wako ni upi katika kazi?

JIBU: Mimi huwa naelewa na kufundishika kwa haraka na ni mchapakazi wa kweli.

 

SWALI: Unapenda nafasi au cheo gani katika timu unayofanya nayo kazi?

 

JIBU: Haijalishi hadi nitakapojifunza kitu kipya kwa kila mradi au kazi.

 

SWALI: Je, unaswali lolote kwetu?

 

JIBU: Lini naweza kujiunga nanyi?

MWISHO

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles