27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

FAMILIA YAMHURUMIA KYLIE JENNER

NEW YORK, MAREKANI


FAMILIA ya mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Kylie Jenner, imeweka wazi kuwa inamhurumia staa huyo kupata ujauzito akiwa na umri mdogo.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 20, anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza Machi mwaka huu pamoja na mpenzi wake ambaye ni rapa Travis Scott.

Familia ya Kardashiani imesema mrembo huyo bado ni mdogo kwa kuitwa mama, lakini wataendelea kuwa pamoja na kumsapoti mara baada ya kujifungua.

Dada wa mrembo huyo, Kim na Kourtney Kardashian, wamedai kuwa wanatumia muda wao mwingi kujaribu kukaa pamoja ili kumshauri maisha ya uzazi, huku wakisaidiana na mama yao Kris Jenner.

Lakini inadaiwa kwamba mama huyo ana furaha kubwa kuona mwanaye ana ujauzito kwa madai kwamba anapenda sana wajukuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles