26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Nameless: Wasichana pendeni nyimbo zangu si mapenzi

Nameless-David-MathengeNAIROBI, KENYA

STAA wa muziki nchini Kenya, David Mathenge (Nameless), amesema ubora wa nyimbo zake unasababisha apendwe na idadi kubwa ya wasichana warembo waliopo nchini humo bila kujali kwamba ni mume wa mtu.

Alisema ingawa asilimia 80 ya nyimbo zake ‘Juju’, ‘Deadly’ na ‘Butterfly’ hulenga wasichana, waishie kuzipenda nyimbo hizo na si zaidi ya hapo kwa kuwa anaiheshimu na kuijali ndoa yake.

“Sina uhakika kama wanapenda kazi zangu tu, kwa kuwa kuna wengine wanaonekana kuwa na maelezo mengi nje ya muziki wangu, lakini wanatakiwa kutambua kwamba nipo kwenye ndoa na nina familia yangu,” alifafanua Nameless.

Msanii huyo amefunga ndoa na msanii wa muziki nchini humo, Wahu na wana takribani miaka 10 ya ndoa yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles