27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Bieber aomba kurudiana na Selena Gomez

justin-bieber-2013-3226-hdwallfan-jpgLAS VEGAS, MAREKANI

MSANII wa muziki wa pop nchini Marekani, Justin Beiber, amesema yupo tayari kurudiana na mpenzi wake wa zamani mwanamitindo, Selena Gomez.

Beiber ataendelea kumkumbuka mrembo huyo kwa kuwa ndiye msichana wake wa kwanza katika maisha yake ya kimapenzi huku akidai kwamba wamefanya mambo mengi walipokuwa wapenzi.

“Kwa sasa najua kila mtu ana mambo yake, lakini kutokana na mambo tuliyofanya wakati wa uhusiano wetu tunaweza kurudiana ila Selena akiwa tayari, lakini kama amepata mpenzi mpya siwezi kuwaachanisha,” alisema Beiber.

Hata hivyo, baada ya wawili hao kuachana, Selena naye alionekana kutoka na wanaume tofauti lakini hajaweka wazi kama yupo katika uhusiano wa kimapenzi na nani kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles