Ali Kiba: ‘collabo’ zitatuvusha kimataifa

0
956

alikibaNA MWANDISHI WETU

MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya Bongo Fleva, Ali Kiba, amesema moja ya mafanikio anayojivunia katika kazi ya muziki kwa mwaka huu ni ushiriki wake katika onyesho la Coke Studio msimu wa tatu.

Kiba, ambaye amefanya kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki wa kike anayetamba nchini Kenya, Victoria Kimani, alisema anajivunia kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaoshiriki maonyesho hayo.

Alisema kuwa ushiriki wake huo umemwezesha kuongeza rekodi yake katika anga la kimataifa na ameweza kujiongezea mashabiki wanaofuatilia onyesho hilo.

“Fani ya muziki inazidi kukua kiasi kwamba wakati wa kufanya muziki wa ndani tupu umekwisha na inabidi kuvuka
mipaka na kufanya kolabo kama hizi, zinasaidia kupata uzoefu na kufungua milango ya mafanikio,”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here