23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mwimbaji wa Kenya afurahia kurekodi video Tanzania

Injili Kenya BettyNA GEORGE KAYALA

MWIMBAJI anayechipukia katika muziki wa injili nchini Kenya, Betty Chepkorir, amedai mazingira na vivutio vingi vizuri vilivyopo Tanzania ndivyo vilivyomfanya arekodi wimbo wake nchini hapa.

Mwimbaji huyo amerekodi video ya wimbo wake wa ‘Nifanye Wako’ mwanzoni mwa mwezi huu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Betty aliliambia MTANZANIA kwamba, wimbo huo utaanza kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga vya nchini Kenya na kampuni ya Afrika Nasaha Production itasambaza wimbo huo kwa vituo vya Tanzania.

“Kampuni yangu ilivutiwa na mandhari ya Tanzania ikanileta Tanzania tukarekodi video hii na tayari umekamilika, ukiwa na mwonekano mzuri na siku za hivi karibuni utaanza kuonekana kwenye televisheni za Kenya, kisha Watanzania nao wataona kupitia runinga zao,” alieleza mwimbaji huyo.

Afrika Nasaha Production ni kampuni inayojishughulisha na shindano la kuwatafuta waimbaji wenye vipaji walio vyuoni na mashuleni na washindi hudhaminiwa kwa kulipiwa ada ama kufadhiliwa katika utengenezaji wa kazi zao na Betty ni mmoja wa zao hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles