23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Nikki wa Pili: Bado mimi tu kutoa wimbo wa kimataifa

Nikki wa PiliNA THERESIS GASPER

MSANII wa miondoko ya hip hop kutoka Kampuni ya Weusi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amedai kwamba kwa mwaka huu amejipanga kuachia video za nyimbo zake mbili tu zenye viwango vya kuchezwa kimataifa.

Licha ya kutamka kauli hiyo, bado hajafikiria nyimbo za kuachia kwa mwaka huu kutokana na kuwa na idadi kubwa ya nyimbo alizokwisha ziandaa mwishoni mwa mwaka jana.

“Katika Kampuni yetu wenzangu wote wamefanikiwa kuachia video za kimataifa isipokuwa mimi, hivyo nipo mbioni na mimi kuwapa ladha mashabiki wangu kwa nyimbo hizo zenye kiwango cha kimataifa,” alifafanua.

Alisema lengo ni kuzidi kuwapa mashabiki wake ladha tofauti ili aweze kuliteka soko la muziki wake na pia kuongeza ushawishi kwa vijana wengine ili wachangamkie fursa ya ajira kupitia muziki huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles