22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mwigulu awaonya maofisa uhamiaji

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

NA SAFINA SARWATT, MOSHI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amewataka maofisa
uhamiaji waliopo mipakani waache tabia ya kusindikiza wahalifu na wahamiaji haramu.

Amesema kwamba, mtumishi yeyote atakayebainika akishirikiana na watu hao, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufukuzwa kazi.

Mwigulu alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipofanya ziara ya siku moja mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kujionea njia zisizo rasmi zinazotumiwa na  wahalifu katika wilaya za Rombo na Mwanga.

“Kuna malalamiko yanawahusu baadhi ya maofisa wa uhamiaji na askari polisi kwamba wanahusika kuwasindikiza wahalifu wanaofanya biashara za magendo pamoja na wahamiaji haramu.

“Nawaomba waache mara moja, kama watashindwa, basi wajue watachukuliwa hatua kali pindi watakapokamatwa.

“Ili kuwabaini watu hao, nakuomba wewe mkuu wa uhamiaji wa mkoa, uhakikishe maofisa wanaofanya kazi katika mipaka wanafuatiliwa kikamilifu ili waweze kuchukuliwa hatua kwani wanalichafua Jeshi la Polisi,” alisema Mwigulu.

Katika maelezo yake, Mwigulu alisema wilaya za Rombo na Mwanga zinaongoza kwa kuwa na njia nyingi za panya ambazo zimekuwa zikitumiwa na wahalifu hao.

“Wilaya ya Mwanga ina njia za panya zaidi ya mia tatu. Rai yangu kwamba njia hizo  zidhibitiwe ili kukabiliana na wahalifu hao sambamba na kushirikisha wananchi.

Akizungumzia suala la kukamatwa kwa wasafirishaji wa wahamiaji haramu
na kesi zao kuchukua muda mrefu mahakamani, waziri huyo alisema ameshazungumza na Waziri wa Katiba na Sheria ili kuangalia namna ya kutatua jambo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles