29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mourinho, Guardiola waiteka Manchester

Jose Mourinho and Pep Guardiola
Jose Mourinho and Pep Guardiola

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA mpya wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho na mpinzani wake wa Manchester City, Pep Guardiola, juzi waliliteka Jiji la Manchester baada ya kuwasili kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu.

Juzi kupitia akaunti yake ya Instagram, aliiweka video ambayo ilikuwa inamwonesha kuwasili kwake katika jiji hilo na kuwapa taarifa mashabiki wa timu hiyo ambapo alisema: “Tayari nimetua, kwa pamoja United tunaweza,” alisema Mourinho.

Leo kocha huyo ataonekana kwa mara ya kwanza akiwa na timu tangu alipofukuzwa kazi na Chelsea, Desemba mwaka jana, hivyo ataanza rasmi kuiongoza United kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Mashabiki wa United katika jiji hilo walionekana wakiwa na mabango mbalimbali yakiwa na ujumbe wa kumkaribisha kocha huyo ambaye alitumia saa 2:47 kutoka nyumbani kwake jijini London hadi United.

Tayari Mourinho ameanza kufanya usajili kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya huku akiwa amewasajili, Eric Bailly, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.

Wakati huo kwenye Uwanja wa Etihad, mashabiki wa Manchester City walijitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumuona kocha wao, Pep Guardiola ambaye aliwasili siku hiyo.

Kocha huyo aliitaja mikakati yake ndani ya klabu hiyo ambayo iliwafanya mashabiki kuwa na furaha kubwa huku wakiamini kwamba wamepata mkombozi wao kwa kipindi hiki.

“Najua watu wengi wamejitokeza hapa si kwa ajili ya kuja kuniona, ila ninaamini wamejitokeza kwa lengo la kutaka kuwaona wachezaji wao.

“Kwa sasa siangalii mwaka huu kwamba nitafanya nini, ila ninachokiangalia nitakutana na changamoto gani, England kuna makocha wenye uwezo mkubwa hivyo lazima nijipange vizuri.

“Makocha ambao ni wazuri ni pamoja na Jose Mourinho, Jurgen Klopp, Antonio Conte, Claudio Ranieri, Mauricio Pochettino, Ronald Koeman, lakini nimeamua kujiunga na timu hii kwa ajili ya kusaidia wachezaji pamoja na kuipa mataji timu hii.

“Natarajia kukutana na wachezaji kwanza kwa ajili ya kuwajua vizuri, siku zote nimekuwa nikiwajua kutokana na kuwaona kwenye runinga, hivyo ninahitaji kupata muda wa kuwa nao,” alisema Guardiola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles