23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti CCM mbaroni kwa ulevi

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Busega, George Mshoni amekamatwa na polisi mkoani Simiyu akidaiwa kulewa saa za kazi.

Akizungumza na MTANZANIA  kwa   simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga alithibitisha kukamatwa kwa mwenyekiti huyo.

“Ni kweli tumemkamata na kumtia mbaroni Mshoni kwa   kukutwa akiwa amelewa saa za kazi, tulipata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa mwenyekiti huyo alikuwa amekaa baa akipata kilevi.

“Askari walikwenda na kumkuta akiwa amelewa, walimkamata …sina hakika kwa sababu sipo ofisini kwa sasa lakini leo (jana) ilikuwa afikishwe mahakamani,” alisema.

Lyanga alikamatwa jana akiwa katika baa yake katika Kijiji cha Masanza Kona wilayani humo saa 8.00 mchana akiwa amelewa.

Tangu kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya tano Novemba, mwaka jana, Rais Dk. John Magufuli amekuwa akiwataka watanzania kuzingatia muda wa kufanya kazi ili kuinua uchumi wa nchi na wao binafsi.

Katika kutilia msisitizo suala hilo, Rais Magufuli alipiga marufuku mchezo maarufu wa ‘Pool table’ ambao alisema umekuwa ukiwafanya watu wengi hasa vijana, kushindwa kuzingatia kufanya kazi na kushinda wakicheza na kulewa.

Katika kulisimamia hilo, Mei 20, mwaka huu alitengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kwa kuingia bungeni na kujibu swali huku akiwa amelewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles