23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanza iko tayari kwa uwekezaji wa Kimataifa-RC Gabriel

* Asema zaidi ya  Sh bilioni 339 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia

Na Clara Matimo, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amesema kutokana na miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali mkoani humo.

Akizungumza jijini Mwanza leo Aprili 6, 2022 wakati wa kuzungumzia mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Madarakani, amesema kwa sasa mkoa huo umefunguka na uko tayari kwa fursa kubwa za uwekezaji wa kimataifa.

Aidha, ameonya kuwa chini ya uongozi wake mkoa huo hautakuwa sehemu ya vikwazo vya kukwamisha miradi na malengo mazuri ya serikali katika kupiga hatua na kuboresha maisha ya wananchi wake.

Baadhi ya wafanyakazi, wageni waalikwa na wananchi wa Mkoa wa Mwanza, wakisikiliza taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa  mkoani humo ndani ya siku 365 za uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Mkoa wa Mwanza kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhun Hassan tumepokea jumla ya Sh bilioni 339, 655, 579,831  kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kimkakati, ikiwemo upimaji wa ardhi ambapo baada ya serikali kuleta fedha za upimaji ardhi kuna viwanja kando ya mwambao wa Ziwa Viktoria ambavyo vinafaa kwa uwekezaji wa hoteli za kimataifa kwani mkoa huu uko  karibu na mbuga ya wanyama ya kimataifa Serengeti.

“Mwanza kwa sasa ni sehemu salama ya kuwekeza Afrika mashariki kwa sababu ina ardhi kubwa na mkoa wa pili kwa kuchangia pato la taifa baada ya Dar es Salaam, tuna uwezo mkubwa wa kuleta mapinduzi… watu wameshaona fursa za kuwekeza katika mkoa wetu kutokana na uwekezaji unaoendelea.

“Mwanza imeiva kiuchumi, Mwanza imefunguka kiuchumi na kiuwekezaji, Mwanza hatutakuwa sehemu ya kukwamisha mikakati na nia njema ya serikali katika kupiga hatua za maendeleo,” amesema Mhandisi Gabriel.

Aidha mkuu huyo wa mkoa  ameendelea kufafanua miradi mingine iliyotekelezwa ndani ya mkoa huo kuwa ni  ujenzi wa stendi ya mabasi Nyamhongolo ambao umekamilika kwa asilimia 100, Stendi ya Nyegezi, soko la kisasa, meli ya kisasa ya biashara, Daraja la Busisi (asilimia 40),  huku akibainisha kwamba miradi hiyo itazidi kuutangaza mkoa huo  kimkakati na kuufungua kimataifa.

“Ndani ya mwaka mmoja wa rais wetu mpenda wananchi wake, tumepokea Sh bilioni 42 kwa ajili ya miradi ya afya ikiwemo Sh bilioni 10.8 kujenga hospitali za halmashauri za Wilaya  za Buchosa, Sengerema, Ilemela, Misungwi, Kwimba, Sh bilioni 3.75 ujenzi vituo vya afya 10 kikiwemo kituo cha Kayenze ambacho mtoto wa kwanza wa kiume alizaliwa akapewa jina Kayenze, Sh bilioni 4.9 kuboresha miundombinu, majengo ya huduma za kibingwa na vifaa tiba hospitali ya  Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando na Sh Bil 2.7 upanuzi hospitali ya Nansio iweze kutoa huduma za kibingwa.

“Upande wa elimu  Sh bilioni 20.5 zimetumika kujenga vyumba 385 vya madarasa na vyote vimeishakamilika tumebakiza Sh milioni 800 ambazo tumezitumia kujenga ofisi 51 za walimu, matundu 81ya vyoo, maabara 20 na thamani zingine, Sh bilioni 4.5 ujenzi wa vyuo vya ufundi Wilaya za Ukerewe na Kwimba, mkoa una jumla ya vyuo vikuu 7 vyenye wanafunzi 9430, vyuo vya kati 36  wanafunzi 14620.

Amesema upatikanaji wa maji mjini ni asilimia 88, vijijini asilimia 65 na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (Mwauwasa)  hadi Machi mwaka huu imepokea Sh bilioni 29.7 kwa ajili ya usambazaji maji.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa usimamizi mzuri wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka  2020-2025.

“Niwaombe viongozi wa Serikali, idara zilizopo mkoani kwetu na wale wa chama cha Mapinduzi tujitahidi kupeleka taarifa kwa wananchi ambako miradi inafanyika kuwaeleza kinachofanyika maana bado yapo mengi ya kufanyika na miaka tunayo mitatu kwa ushirikiano huu tutafanya kazi kubwa sana,” amesema Diallo.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ngussa Samike, amesema”
Kwa niaba ya watumishi tunaahidi kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu  na kujituma  ili kuuletea maendeleo mkoa huu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Hassan Masalla, amesema wilaya hiyo ndiyo manispaa pekee yenye eneo kubwa la kimkakati na ambalo limepimwa hivyo wanawakaribisha wadau mbalimbali kwenda kuwekeza katika ardhi na ujenzi wa hoteli kwenye fukwe.

Mwakilishi wa vyama vya siasa, Holela Mabula, kutoka Chama cha Kijamii (CCK),amesema ndani ya siku 365, Rais Samia Suluhu Hassan, mejipambanua kwa kufanya mambo mbalimbali yenye  manufaa kwa  taifa na wananchi kwa ujumla ikiwemo katika sekta ya kilimo na kuimarisha mahusiano ya Kimataifa.

 “Ombi langu kwa Rais Samia Suluhu Hassan, wavuvi wa visiwani ndani ya mkoa huu  wakumbukwe kwa kutengenezewa korido za kukaushia dagaa (kuanika) ili kuzalisha dagaa wenye ubora wasio na mchanga ambao wanaweza kuuzwa nje ya nchi pia ushauri kwa mkoa  ujikite kwenye Mapinduzi ya kilimo kwa kuendesha makongamano yatakayoibua mijadala na mapendekezo mazuri ili kuleta tija katika sekta ya kilimo,” amesema Mabula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles