23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kulitazama upya kundi la vijana

*Yazindua mpango wa kuwalinda vijana

*Unalenga kuhamasisha vijana kushiriki katika fursa mbalimbali zikiwamo za kiuchumi

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Serikali imesema kuwa ni ngumu kwa taifa kuwa na maendeleo huku kundi la vijana likiwa limeachwa nje hivyo, imeanza kufanyia mapitio ya sera ya vijana itakayowawezesha kushiriki katika fursa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi katika taifa.

Kauli hiyo ya Serikali inakuja wakati hitaji la mabadiliko ya sera hyo likihitajika zaidi kwa ajili ya ustawi wa vijana.

Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA Tanzania, Mark Bryan Schreiner, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika Dar es Salaam Aprili 4, 2022. Picha -UNFPA.

Kwani Vijana wanaamini kuwa sera iliyopo hivi sasa haiwapi nguvu kubwa ya uwakilishi wao kwenye masulaa mbalimbali.

Hayo yameelezwa Aprili 4, 2022 na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa kuboresha ustawi wa Vijana (SYP) unaodhaniniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu na Afya ya Uzazi (UNFPA).

Naibu Waziri Katambu amebainisha kuwa mapitio ya sera hiyo yanalenga kutoa mwanya kwa vijana kuzifikia fursa za uchumi, uongozi na kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.

“Sisi kama Serikali tuna amini ndani ya awamu hii ya sita sera ya vijana itapatikana. Tayari tumeanza kufanya maboresho yatakayotoa fursa kwa vijana kushiriki moja kwa moja kwenye shughuli za kuuchumi na kujiletea maendeleo.

“Kwani hatuwezi kuwa na taifa ambalo maendeleo yake yataacha kundi la vijana nje, hivyo kwa kutambua kuwa kundi hili la vijana ndilo lenye idadi kubwa kwa mujibu wa makadirio ya watanzania, hivyo juhudi zinafanyika kuona maboresho makubwa yanatokea,” amesema Katambi.

Katambia amefafanua zaidi kuwa, sera hiyo iliyotungwa mwaka 2007 imeshajadiliwa na timu ya wataalamu na sasa inatarajiwa kupelekwa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba linaloanza Jumanne hii ya Aprili 5, kwa ajili ya hatua zaidi.

Ikumbukwe kuwa sera ya inayotumika sasa ambayo iliundwa zaidi ya miaka 10 iliyopita imepitwa na wakati ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya vijana na mabadiliko na nchi kwa ujumla.

Sera iliyopo sasa inatajwa kuwa na mapungufu kadhaa, ikiwemo kutogusa maslahi ya vijana.

Katambi aliongeza kuwa katika sera hiyo mawazo ya vijana yatahusishwa kuhakikisha inagusa maeneo yote na kuwa msingi wa uwezeshaji kwa vijana.

Amese jukumu la serikali kwa sasa ni kubadili mitazamo ya vijana ili wawe na malengo na uwezo wa kuyasimamia.

“Kila kijana anapaswa kutafakari anataka kusaidia taifa kwa namna gani na wajibu wa serikali ni kutengeneza mazingira wezeshi,” amesema Katambi.

Kuhusu programu hiyo, Katambi amefafanua kuwa itasaidia juhudi za kuwawezesha vijana wawe na mchango chanya kwa taifa.

Akizungumza kuhusu mpango huo, Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Mark Schreiner, amesema ulianza mwaka 2013 katika nchi za Kusini mwa Afrika na sasa utatekelezwa nchini kwa Mikoa mitano ya awali ikiwamo mikoa ya Unguja na Pemba.

Amesema kuwa mpango huo unawalenga vijana wa miaka 10 hadi 24 ambao ni rika la kubarehe na inatekelezwa katika Mikoa mitano yaani Shinyanga, Kigoma, Simiyu, Dodoma na Dar es Salaam huku Zanzibar ukitekelezwa Pemba na Unguja yote kwa gharama ya Sh 14.3 bilioni.

Upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Zlatan Milicic, amesema ni furaha kubwa kuona mpango huo umezinduliwa nchini Tanzania na anaamini kuwa uteleta manufaa makubwa kama ilivyo matarajio yao.

“Kama ilivyoelezwa na na watangulizi wangu, kwamba Mpango wa SYP umekuja kwa wakati muafaka ambapo UNFPA itazindua na kutekeleza Mpango wao wa 9 wa Nchi; na vile vile Mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, pamoja na Serikali utazindua Mfumo wetu wa Ushirikiano Endelevu wa Umoja wa Mataifa (UNSDCF) 2022-2027 uliosainiwa hivi karibuni.

“UNSDCF inatoa mfumo wa msaada wa UN kwa Tanzania ili kufikia vipaumbele vya maendeleo ya taifa kama ilivyoangaziwa katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026, Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na matarajio ya kikanda na ahadi ikiwa ni pamoja na Ajenda ya Afrika 2063.

“Pia UNSCDF inaweka vijana katikati ya ajenda ya maendeleo. Maeneo manne ya kipaumbele ya kimkakati ya UNSDCF yaliandaliwa kwa kuzingatia uchanganuzi wa mazingira ya maendeleo ya Tanzania ambao uliwezesha kubainisha maeneo ambayo Umoja wa Mataifa una nafasi nzuri zaidi ya kutumia faida zake linganishi ili kuharakisha maendeleo ya vipaumbele vya maendeleo ya taifa na SDGs.

Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA Tanzania, Mark Bryan Schreiner(katikati) akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa mpango huo.

“Maeneo hayo ni pamoja na kuimarisha huduma za kijamii zinazowawezesha wanawake na wasichana; kubadilisha uchumi; kuimarisha mifumo ya utawala wa kitaifa; kujenga ustahimilivu na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi miongoni mwa mengine mengi.

“Kama familia Moja ya Umoja wa Mataifa, tumesikia sauti za vijana na mwelekeo mpya wa Mpango wa Ulinzi wa Vijana katika Kanda ya SADC na ESA – na sasa nchini Tanzania – na ninaamini kwamba masuala yote yaliyotajwa na kujadiliwa yameingizwa ndani, vipaumbele vinne vya kimkakati vya Mfumo wa Ushirikiano Endelevu wa Umoja wa Mataifa (UNSDCF) 2022-2027. Mpango wa SYP kwa hivyo ni mpango wa thamani sana na unaowiana wa kusaidia utoaji wa UNSDCF yetu mpya, na kuwasaidia vijana kote Tanzania kufikia uwezo wao kamili,” amesema Milicic.

Akielezea mafanikio yaliyopatikana katika mpango uliotangulia kwenye nchi zilizoko kusini mwa Afrika, Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA Tanzania, Mark Bryan Schreiner amesema kuwa ni pamoja na wanachama 14,500 wa mtandao wa vijana waliopewa uwezo wa utetezi wa ASRHR.

“Pia walimu 31,000 wa shule waliofunzwa kuhusu elimu ya kujamiiana (CSE) kupitia mtandao na mbinu za ana kwa ana, aidha, zaidi ya vijana Milioni 21 waliofikiwa na programu za mawasiliano ya mabadiliko ya tabia ya kijamii (SBCC).

“Wahudumu 13,000 wa huduma ya awali na watoa huduma za afya wakiwa kazini waliopata mafunzo ya utoaji wa huduma bora za afya kwa vijana na vijana (AYFHS), vituo 801 vya kutolea huduma za afya zimetumika katika kutoa kifurushi cha kawaida cha AYFHS katika maeneo ya mradi pia vijana na vijana milioni 8 waliofikiwa na huduma za ASRHR na VVU,” amesema Schreiner .

Amefafanua zaidi kwa kusema kuwa upande wa Tanzania, wanafahamu vyema changamoto ambazo bado zinapaswa kufanyiwa kazi zikiwamo suala la elimu, afya na ustawi wao.

“Bado kuna viwango vya juu vya mimba za utotoni (27%), ndoa za utotoni (37%), maambukizi ya VVU kwa vijana 15-24 (1.4%). Pia tunajua kwamba ukatili wa kijinsia, kimwili, kihisia na kisaikolojia ni aina ya ukatili wa kawaida unaoathiri vijana kote nchini huku asilimia 50.3 ya vijana (15-24) walipata ukatili wa kijinsia,” amesema Schreiner.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles