24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Mwandishi gazeti la Mseto mbaroni

Josephat Isango
Josephat Isango

Na Asifiwe George, Dar es Salaam

MWANDISHI wa habari wa gazeti lililofungiwa la Mseto, Josephat Isango, anashikiliwa na polisi kutokana na habari aliyoiandika yenye kichwa cha habari ‘Waziri amchafua JPM’ la  Agosti 4  hadi 10 mwaka huu.

Isango alifika kituoni hapo saa 5 asubuhi akiwa ameongozana na mwanasheria wake Fredrick Kiwhelo.

Baada ya kukaa katika ofisi ya mpelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa saa sita kwa ajili ya mahojiano waliondoka na kwenda katika ofisi zao zilizopo Kinondoni kwa ajili ya ukaguzi.

Askari watatu pamoja na mwandishi huyo wakielekea katika ofisi hizo walitumia gari mbili zenye namba za usajili T 437 BWX na T 805 BHY zote aina ya Tax.

MTANZANIA lilipomtafuta Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Hezron Gyimbi ili azungumzie tukio hilo alisema yupo kwenye kikao  angetoa taarifa kuhusu tukio hilo.

Agosti 11, mwaka huu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alitangaza kulifungia gazeti la Mseto kwa miaka mitatu, kutokana na kuandika habari ya uongo kwa kutumia nyaraka za kughushi.

Nape aliwaambia waandishi wa habari kuwa, uamuzi huo umetolewa kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 Sura 229 kifungu 25 (1).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles