25 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAMKE MWENYE ASILI YA TANZANIA ATEULIWA MBUNGE PAKISTAN

Sindh, Pakistan

Mwanamke wa kwanza kutoka Afrika mwenye asili ya Tanzania, Tanzeela Qambrani, ameteuliwa kuwa mbunge nchini Pakistan.

Qambrani (39) aliteuliwa na chama cha Pakistan People’s Party (PPP) cha Waziri wa zamani Benazir Bhutto kutumikia kiti maalumu kwa wanawake kwenye bunge la mkoa wa Sindh kusini mwa India.

Uteuzi wa Qambrani umefufua matumaini kwa watu wa jamii ndogo na maskini wenye asili ya Afrika nchini humo.

Qambrani ana matumaini kuwa uteuzi wake utasaidia kuondoa ubaguzi ambao umekuwepo dhidi ya jamii ya Sidi, jina wanaloitwa watu wenye asili ya Afrika wanaoishi maeneo ya pwani ya Makran na Sindh nchini Pakistan.

“Kama jamii ndogo iliyopotelea kwenye jamii kubwa za wenyeji, tumekuwa na wakati mgumu kudumisha tamaduni zetu za Afrika, lakini ningependa kuona kuwa jina Sidi linakuwa lenye heshima,” alisema Qambrani

Qambrani akiwa amevaa mavazi ya kiafrika, aliapishwa Jumatatu wiki hii na amenukiliwa akisema alijihisi kama aliyewahi kuwa rais na mkombozi wa taifa la Africa Kusini, Nelson Mandela.

Pamoja na mambo mengine, watu wengi wa jamii ya Sidi walitokana na watumwa waliopelekwa India kutoka Afrika Mashariki na Wareno.

Walishika nyadhifa za juu wakati wa utawala wa Mughal lakini wakatengwa sana chini ya ukoloni wa Mwingereza.

Hata hivyo hakuna mtu kutoka jamii ya Sidi aliwahi kuingia bungeni hadi Bhutto Zardari, alipomteua Qambrani kwenye kiti maalum.

Kwa upande wake Qambrani, ni mtaalamu wa masuala ya kompyuta ambapo ana shahada ya uzamili katika somo la kompyuta kutoka chuo kikuu cha Sindh, Jamshoro.

Ameolewa na amejaliwa watoto watatu. Baba yake Abdul Bari alikuwa ni wakili na mama yake ni mwalimu mstaafu.

Familia yake imedumisha uhusiano wake na Afrika mmoja wa dada zake aliolewa nchini Tanzania.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles