24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

BODI YA LIGI KUANZA BILA MDHAMINI

LULU RINGO


Ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 22, imemaliza mkataba wake na mdhamini wake mkuu Vodacom na sasa ligi hiyo itaanza bila kuwa na mdhamini mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu (TPBL ), Boniface Wambura amesema ligi itaanza bila mdhamini mkuu hivyo timu zote zitajitegemea vifaa hadi atakapopatikana mdhamini mkuu.

“Mkataba na Vodacom umekwisha hivyo tunatarajia kuanza ligi bila mdhamini lakini tuna mazungumzo na baadhi ya makampuni na mdhamini wetu wa awali naye tunazungumza naye kama tutafikia muafaka,” amsema Wambura.

Aidha mkurugenzi huyo ametolea ufafanuzi kuhusu suala la timu zinazoshiriki ligi hiyo msimu wa 2018/19 ambapo amesema timu hizo itabidi zijitegemee katika majukumu yote yaliyokuwa yakifanywa na mdhamini wa ligi hapo awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles