24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAJESHI JWTZ AUAWA NA MCHUMBA WAKE


Na ELIZABETH KILINDI-NJOMBE -

ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha 514 KJ Makambako, Neema Masanja (25), amefariki dunia kwa kupigwa risasi na mchumba wake, Zakayo Dotto (25),  mwenye namba H. 2299 ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi.

Askari huyo mkazi wa Mtaa wa jeshini Kata ya Maguvani mkoani Njombe aliuawa nyumbani kwake na anayedaiwa kuwa ni mchumba wake ambao walikuwa wanatarajia kufunga ndoa Juni, 2018.

Tukio hilo lilitokea jana saa 12:20 asubuhi wakati marehemu huyo alipokuwa anajiandaa kwenda kazini ndipo mpenzi wake huyo aliingia nyumbani akitokea lindo akiwa na bunduki ya SMG.

Taarifa zaidi zinadai kwamba kulitokea ugomvi baina ya wawili hao uliosababisha Neema kupigwa risasi mbili na kufariki dunia papo hapo.

Shuhuda wa tukio hilo Asty Lusambo, alisema walisikia mlio wa risasi mbili muda huo na walipochungulia dirishani walimwona mdogo wa marehemu akikimbia huku akisema dada ameuawa.

Alisema baada ya kusikia kelele hizo mama mwenye nyumba Sophia Manyika alimfuata yule binti alipokimbilia lakini hakumwona, hivyo aliamua kurudi kwenye chumba cha marehemu na kukuta mwili ukiwa chini.

“Baada ya kusikia makelele, mke wangu akamfuata ila hakumwona ikabidi arudi ndani, yaani chumbani kwa marehemu na kukuta mwili ukiwa chini huku damu zikichuruzika,” alisema Lusambo.

Naye Christian Kinyaga, alisema marehemu na askari huyo wote wana………….. Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles