25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mwanafunzi darasa la tatu apata ujauzito

Hadija Omary – Lindi

NI maajabu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwanafunzi wa darasa la tatu wa Shule ya Msingi Pangatena kupata ujauzito.

Mwanafunzi huyo ambaye jina limehifadhiwa, ni miongozi mwa wanafunzi 40 waliopata ujauzito katika Wilaya ya Kilwa mkoani hapa mwaka huu.

Kati ya wanafunzi hao ambao wamelazimika kukatisha masomo, wamo wa shule za msingi na sekondari.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo. Christopha Ngubiagai juzi alipozungumza na wananchi wakati wa sherehe ya kumbukizi ya miaka 114 ya vita ya Majimaji iliyopiganwa mwaka 1905-1907 wilayani humo.

Ngubiagai alisema takwimu hizo ni kuanzia Januari hadi Julai, mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo, Ngubiagai aliwaasa wazazi na walezi kuendeleza mapambano dhidi ya janga hilo kubwa na kuvitaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.

Alisema ni ajabu kuona Kilwa inaongoza kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaokatishwa masomo, licha ya Serikali kuweka nguvu kubwa ya kutokomeza mimba za utotoni.

“Tarafa ya Pande ndiyo inayoongoza kuwa na mimba nyingi kwa wanafunzi. Kila mwezi huwa na mwanafunzi mmoja aliyekatisha masomo.

“Serikali inachukua hatua kali kali, lakini kuna watu hawasikii. Katika hili nawaambia tutapambana nalo kila siku,” alisema.

Ngubiagai alisema hadi sasa, wanafunzi saba ndani ya tarafa hiyo wamepata ujauzito, watatu wa shule ya msingi na wanne sekondari.

Alisema miongoni mwa watu wanaotajwa kuongoza kushiriki mapenzi na kuwajaza mimba wanafunzi, ni walimu na madereva bodaboda.

Alitolea mfano Kata ya Namayuni inayoongoza kwa walimu kushiriki uhusiano wa mapenzi na wanafunzi wao.

Alisema ni jambo la aibu kuona kama wazee walipambana na wakoloni wakaamka, leo wanaona vijana wanapambana kuwatia mimba watoto.

“Kama wazee wetu walipambana kumwondoa mkoloni na wakamwaga damu, vijana tunao wajibu wa kuwasaidia watoto wa kike wasipate ujauzito wakiwa na umri mdogo.

“Ni jambo la aibu, wazee wetu wakiamka leo wakaona  haya mambo sidhani kama watatuelewa.

“Wakuu wa wilaya wenzangu wananiuliza Kilwa kuna nini maana kila kidume kinafukuzia katoto, ndugu zangu mnanitia aibu tafuteni saizi zenu mkamalizane,” alisema Ngubiagai.

Alisema Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yeyote atakayebainika kumpa mimba mwanafunzi ama kushiriki naye mapenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles