30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

NGO 158 zafutiwa usajili

Mwandishi Wetu- Mbeya

MSAJILI wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), Vickness  Mayao, ameyaondoa mashirika zaidi ya 158 katika rejista ya mashirika yasiyo ya kiserikali.

Hayo yamesema jijini Mbeya na Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa NGOs kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Grace Mbwilo kwa niaba ya mkurugenzi na msajili wa NGOs.

Alisema Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya mwaka 2002,  kama ilivyofanyiwa mabadiliko  na Sheria  Namba 3 ya mwaka  2019, imefafanua bayana kuwa jukumu  la kusajili mashirika yanayoendesha shughuli za kijamii, kiutamaduni, kiuchumi, utawala bora, haki  za  kibinadamu na  mazingira   katika  ngazi  ya  jamii  kwa  lengo  la kutogawana faida  na  ambazo hazina mrengo wa  kukuza  biashara, zimeelekezwa kusajililiwa na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs).

“Mashirika   yaliyoondolewa   kwenye   daftari    la msajili   wa   NGOs   ni   yale   ambayo yalisajiliwa chini  ya sheria  ya mashirika yasiyo ya kiserikali Na.  24   ya mwaka 2002 ambayo yanafanya kazi kwa   lengo  la kunufaisha wanachama wake, kugawana faida, yenye   mlengo  wa   dini,  yenye   lengo   la  kukuza   biashara  na  bodi  za   wadhamini,” alisema Grace.

Alisema hatua ya kuyaondoa mashirika haya  kwenye  daftari, imefikiwa kwa mujibu wa Sheria ya Marekebisho Na. 3 ya mwaka 2019 iliyoanza  kutekelezwa  kuanzia  Julai mosi, mwaka huu.  

Grace alisema kwa kuzingatia ufafanuzi wa  mipaka ya  usajili ulioainishwa na  Sheria  Namba 3  ya Mwaka   2019, msajili  wa  NGOs,  anayakumbusha mashirika yanayofanya shughuli kwa lengo  la kugawana faida, yenye mrengo wa dini na ambayo yana  malengo ya kukuza  biashara, yatafutwa kwenye  daftari  la  msajili, na baada ya kipindi cha  miezi miwili  kuanzia Julai mosi, mwaka huu, yatahamishiwa  chini  ya mamlaka  nyingine  za usajili kutokana na kukosa sifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles