30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwana diaspora Loveness azidi kuwasaidia wenye uhitaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi ya Loveness Foundation (LF) imeanzishwa mwaka 2021 nchini Marekani chini ya kifungu cha sheria namba 501 (c) (3) kwa ajili ya kuboresha maisha ya jamii ya Waafrika waliosahaulika wanaoishi maeneo ya vijijini na Marekani.

Maofisa wa Taasisi ya Loveness wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) baada ya kuwapatia msaada wa miwani ya jua na mafuta maalumu ya kutunza ngozi zao katika tukio lililofanyika Dar es Salaam hivi karibuni.

Taasisi hiyo inafanya kazi kupitia mpango mkakati wake wa miaka mitano kuanzia mwaka 2022/2026 unaojumuisha na kuelezea dhima, maono, vipaumbele, majukumu, malengo na misingi ya utendaji wake.

Vilevile, mpango huo umeanza na uchambuzi wa ukweli unaojiri Afrika na mazingira yake unaoshawishi mipango mbadala.

Pia umejikita katika Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) kupitia Ajenda ya mwaka 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Akizungumza hivi karibuni kutoka Marekani, Rais na Mwanzilishi wa LF, Loveness Mamuya, amesema lengo la taasisi yake ni kuwawezesha na kuwashawishi wanawake, wazee, watoto na vijana.

“Taasisi ya Loveness nimeianzisha kwa malengo mahsusi ya kuwasaidia watu wote au jamii ya watu wenye uhitaji kupitia makundi yao maalumu. Kupitia taasisi nawasaidia watu wa makundi hayo maalumu si kwa sababu ya vile walivyo au kwa sababu ya kile wanachokifanya, hapana. Nafanya hivyo kwa saababu hivyo ndivyo tunavyotakiwa kuwasaidia watu wenye mahitaji,” amesema.

Loveness ambaye ni Mtanzania anayeishi nchini Marekani amesema lengo jingine la taasisi yake ni kuboresha maisha ya watu hao kwa kuangazia uzalishaji wa vipato vyao, afya, elimu, mazingira safi na haki jamii.

Kupitia msukumo wake na kuvutiwa binafsi na masuala ya afya na ujasiriamali, Loveness, amejikita zaidi kusaidia mashirika na vikundi vidogo na vya kati vya Tanzania na nje ya nchi.

Mwana diaspora huyo pia anaamini kwamba afya ni jambo muhimu katika ukuaji, maendeleo na ushiriki wa mambo mbalimbali yanayojiri duniani na kupitia kujifunza ujuzi kwa ajili ya kutafuta njia za kutimiza malengo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles