30.4 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wachezaji Yanga: Tuko tayari kuhesabiwa, kwa maendeleo ya wananchi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wachezaji wa Klabu ya Yanga, wamewasihi wapenzi wa soka nchini na Watanzania wote kwa ujumla kushiriki zoezi la Sensa litakalofanyika Agosti 23, 2022.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakiwa Kambini kwao AVIC Town Kigamboni, wao kama wachezaji watamuunga mkono Rais Samia kushiriki zoezi la kuhesabiwa.

Feisal Salum.

“Mimi Feisali Salum mchezaji wa Yanga, napenda kuwajulisha wananchi wote na wapenzj wa mpira wajiandae kuhesabiwa Agosti 23, 2022,” amesema Feisali Salum

Kwa upande wake beki Mahiri wa Yanga Dickson Job amewataka vijana wote kushiriki zoezi hilo la Sensa kwa manufaa yao.

“Napenda kuwashauri vijana wenzangu, waweze kujitokeza kwa wingi siku ya Agosti 23, 2022, Sensa kwa maendeleo ya Watanzania,” amesema.

Wakati huuohuo Mshambuliaji wa Kimataifa wa Timu hiyo, Fiston Mayele amewahasa Watanzania wote bila kujali tofauti zao mbalimbali washiriki zoezi hilo la Sensa ili waweze kupata maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles