33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Pakistani kinara wa unyanyasaji, utekaji, ubakaji wanawake

WAKATI Dunia ikihubiri haki na usawa wa kijinsia huko nchini Pakistani wanawake wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kijinsia , kubakwa na kutekwanyara, anaandika Faki Ubwa …(endelea)

Ripoti mbalimbali nchini humo zimekuwa zikionyesha namna nchi hiyo inavyoshindwa kudhibiti matukio hayo mpaka kusababisha idadi ya wanawake kutekwa kufika 157 huku 112 wakishambuliwa na wengine 91 kubakwa kwa kipindi cha mwezi Juni mwaka huu.

Chombo cha Habari cha The News Internation On Sunday (TSN) kimeripoti tukio la kushambuliwa kwa Mwanablogi (Mwanahabari za mtandao) wa Kimarekani Arablea Urpi huku Dera Ghazi Khan huku mtuhumiwa akidaiwa kutoroka mikononi mwa Polisi na kwamba tukio hilo limetajwa kuwa ni muendelezo wa ukatili kwa wanawake nchini humo,

Urpi ni Mwanablogi anayechapisha na kupakia video zinazohusu safari zake za kitalii kwenye Mtandao wa TikTok.

Urpi alisema kuwa alikuwa katika eneo hilo kwa ajili kutembelea Milima ya Fort Munro ambapo Muhammad Muzammil Sipra na Azan Khosa walimbaka huku wakimrekodi video kwa ajili ya kumdharirisha.

Urpi Alieleza kuwa usiku wa tarehe 17 kuamkia tarehe 18 Julai mwaka huu kwenye chumba cha hoteli alibakwa na watuhumiwa hao “Muzmal Sipra na Azan Khosa walininyanyasa kingono kwenye chumba cha Hoteli ya Anmol “.

Mwanablogi huyu alifanya mawasiliano na Muzmal Sipra kwa ajili kumfikisha eneo la Dera Ghazi Khan kwa ajili ya kufustilis mila za Baloch kama ambavyo wafuatiliaji wake walivyopendekeza.

Upri alinukuliwa akisema kuwa kwenye safari yake alianza Lahore hadi Rajanpur kwa basi na kwamba alifika kwenye makazi ya Sipra aliokaa kuanzia tarehe 13 mpaka 15 Julai ambapo walisafiri pamoja mpaka kwenye Milima ya Fort Munro na kwamba huku ndipo Spira Khosa walitekeleza unyama huo.

Mbali na tukio hilo Vipo Visa vingi vya unyanyasaji wa kijinsi nchini humu pamoja na lile la msichana aliyetekwanyara katika mji wenye hadhi ambapo inazidi kuingia kwenye nafasi ya juu katika orodha ya nchi zenye unyanyasaji wa jinsia na kwamba Serikali ya Pakistani imeingia doa kwa kushindwa kudhibiti matukio hayo kama ambavyo mtandao wa Daily Times ilivyoripoti.

Imeripotiwa kuwa vyombo vya usalama vilitambua tukio hilo kuwa ni tukio la wizi wa gari bila kuhusisha tukio ls ubakaji bila kujali picha za dhahiri za Kamera za CCTV.

Gazeti la The Dawn limechapisha ripoti ya Shirika la Maendeleo Endelevu ya Jamii (SSDO) na Kituo cha Utafiti, Maendeleo na Mawasiliano (CRDC) iliyoonyesha kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake nchini Pakistani.

Serikali kutoshughulikia na matendo hayo kunaongeza matukio hayo na kuifanya nchini hiyo kuwa katika nafasi ya 153 kwenye mataifa yenye ukatili zaidi duniani.

Chanzo: zee5.com

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles