24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mwambe aitaka mikoa kutekeleza miongozo ya uwekezaji

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji, ameitaka mikoa ambayo tayari imeandaa  miongozo ya fursa ya uwekezaji itekeleza kikamilifu kwa kuandaa mikakati ya utekelezaji ikiwamo kutenga maeneo ya uwekezaji na kuyaendeleza.

Waziri Mwambe amebainisha kuwa utekelezaji wa miongozo hiyo utahamasisha na kuvutia uwekezaji katika mikoa hiyo kwa kutangaza fursa za uwekezaji, hali itakayoisaidia mikoa  kujiweka katika nafasi nzuri ya kujitangaza kimataifa kupitia fursa zilizopo nchini.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara yake mkoani Shinyanga, Mwambe amefafanua kuwa utekelezaji wa miongozo hiyo kutaongeza kasi ya wawezekezaji kuja Tanzania na kuwekeza katika maeneo ya vipaumbele vya mikoa husika.

“Mkoa wa Shinyanga  ni miongoni mwa mikoa ambayo imeandaa Mwongozo wa uwekezaji katika sekta ya madini, mazao yatokanayo na mifugo, kilimo na usindikaji wa mazao,”

“Shinyanga ni mkoa ambao kijiografia na kibiashara, upo katika  sehemu nzuri na kuna kila sababu ya kuutekeleza mwongozo wenye kuainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa  huu na kutenga maeneo ya uwekezaji pamoja na  kuyaendeleza ili kuwavutia wawekezaji,” amesema Mwambe.

Katika hatua nyingine,Mwambe ametembelea wawekezaji katika kiwanda cha Jambo Foods Limited na Jielong, ambapo ametoa wito kwa wakazi wa mkoani Shinyanga kuchangamkia fursa za uwekezaji wa viwanda hivyo kwa kulima mazao ambayo yanatumika kama malighafi ya viwanda hivyo.

Amefafanua kuwa Serikali imehamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza nchini na kutumia malighafi za hapa nchini, lengo ni kuhakikisha wananchi wanainuka kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles