25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mwalimu afukuzwa kazi kwa kumshabikia Lowassa

Na Ramadhan Libenanga, Morogoro

MWALIMU wa Shule ya Sekondari Charlotte katika Manispaa  ya Morogoro, Heriman Manase anadaiwa kuachishwa  kazi  akituhumiwa kujihusisha na masuala ya siasa kwa kumshabikia aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayeungwa mkono na vyama vilipo kwenye mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Inadaiwa kwamba mwalimu huyo alikuwa akimpigia  debe Lowassa,  ndani  na nje ya shule hiyo.

Mwalimu huyo pia anadaiwa  kuhudhuria mkutano wa Lowassa jijini Arusha siku mwanasiasa huyo alipotangaza nia ya kugombea urais wakati huo akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

MTANZANIA lilizungumza na mwalimu huyo ambaye alisema uongozi wa shule umemweleza kuwa mkataba wake hautaongezwa utakapomalizika Januari mwakani.

Mwalimu huyo alidai  kuwa uongozi wa shule ambayo ni ya binafsi, ulimweleza kuwa hataongezewa mkataba kwa vile  masomo ya mchepuo wa biashara anayofundisha yamefutwa.

Kwa mujibu wa mwalimu  huyo, Mwalimu Mkuu   wa shule hiyo  aliyemtaja  kwa  jina  la Sr Dorothea Lazaro  alimwita  ofisini kwake na kumwambia  kuwa  bodi ya  shule  imekubaliana kufuta mkataba wake.

Manase alisema mwalimu mkuu alimweleza kuwa   shule  ilikuwa tayari kumlipa  haki zake zote  na  ndiyo maana  hadi  sasa anaendelea  na  kazi  shuleni  hapo  akisubiri  Januari mwakani  mkataba utakapomalizika.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Zakaria John alikataa kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa suala hilo liko polisi, ingawa alisisitiza kuwa   anachojua  yeye  ni kwamba  Manase bado   ni mwalimu  halali  wa shule  hiyo.

Mwalimu   Manase alithibitisha kuwa amekwisha kuitwa  polisi  ambao walitaka   kujua  chanzo  cha barua  hiyo  kusambaa  katika mitandao  ya  jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles