27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Aunguzwa kifuani kwa maji ya maharage

Na Hillary Shoo, Singida

MSICHANA  mmoja amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida, baada ya kumwagiwa maharage ya moto kifuani na dada yake, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Msichana huyo aliyelazwa wodi namba mbili katika hospitali hiyo, ametambulika kwa jina la Tabu Mohamed  (25) ni mkazi wa eneo la Majengo Manispaa ya Singida.

Akizungumza na MTANZANIA huku akiugulia maumivu, Tabu alisema tukio hilo  lilitokea juzi asubuhi, wakati alipokwenda kwa dada yake kwa lengo la kumwomba simu ili atumie kujaza vocha ya kumtumia mama yao.

Hata hivyo alisema katika hali ya kushangaza dada yake huyo aitwae Rehema Jumanne (32), baada ya ombi hilo, hakumjibu chochote na badala yake aliingia jikoni na kupakua maharage ya moto kisha akamwagia.

“Mimi namshangaa dada yangu, ananinunia tu bila sababu yoyote, nikimwuliza hata hasemi chochote, na mimi nimeamua kumwacha kama alivyo,”alisema Tabu bila kuweka wazi sababu ya ugomvi wao.

Kwa upande wake mganga wa zamu aliyemhudumia majeruhi huyo, Dk. Amri Mabelwa, alisema hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri ingawa amekuwa na majereha mwilini.

Kamanda wa polisi Mkoani Singida Thobias Sedoyeka, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema tayari Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa RehemaJumanne, ambaye anadaiwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda Sedoyeka alisema mtuhumiwa akiwa amesimama nyuma ya mdogo wake huyo, ghafla alimwagia maharage hayo kifuani na kumwunguza vibaya sehemu ya shingoni, kifuani na kwenye matiti yake.

“Msichana huyu ameunguzwa vibaya sana kifuani…hadi sasa amelazwa hospitali ya mkoa, wodi namba mbili na madaktari wanaendelea kumtibu,” alisema Kamanda Sedoyeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles