29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 7, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MWAKYEMBE AWAFUNDA WASANII 

NA SALMA MPELI


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amewataka wasanii wa filamu, muziki na kazi nyingine za sanaa kujiunga na Kampuni ya Barazani Entertainment kwa ajili ya uhakika wa kuuza kazi zao.

Akizungumza hivi karibuni wakati akizindua kampuni hiyo, Mwakyembe, alisema kwa muda mrefu wasanii wamekuwa wakilalamika kwa kukosa masilahi katika kazi zao kutokana na kuingiliwa na watu ambao wanajali masilahi yao binafsi.

Alisema kutokana na ujio wa kampuni hiyo ambayo imejikita kwenye kutoa masilahi halisi kwa wasanii, anaamini wakati umefika sasa wa wasanii kuanza kupata masilahi kutokana na jasho lao katika kazi.

Wakati huo huo, Meneja wa uzalishaji na masoko wa Kampuni hiyo, Jacob Steven ‘JB’, alisema Barazani Entertainment itakuwa ni suluhisho kwa wasanii mbalimbali kwani sasa kazi zao hazitauzwa kwenye maduka wala kwa wauzaji wa mitaani, lakini kupitia kampuni hiyo kazi zao zitauzwa kupitia kwenye mihamala ya simu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles