25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

TIMBULO AWATAKA WASANII WAJITEGEMEE

Na BRIGHITER MASAKI


MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Ally Timbulo, amesema wasanii hapa nchini wajifunze kutoa kazi zao kwa kujitegemea si kutegemea wasanii wa nje ambao hawana mchango wowote.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mkali huyo ambaye anatamba na wimbo wa ‘Vibaya’, alisema mfano mzuri kolabo ya Diamond na Davido, ilimtangaza  zaidi Davido hapa nchini kuliko Diamond. .

“Kumshirikisha msanii wa nje nikumleta hapa, tumemjua Davido baada ya kushirikishwa na Diamond baada ya hapo Davido alikuwa kama Mtanzania vile inavyopigwa utasema anatokea Manzese, lakini Davido hakumsaidia Diamond kule Nigeria kuchukua muziki aupeleke kule,” alisema.

Alisema Ali Kiba amefanikiwa kushinda  tuzo bila kolabo na msanii wa nje na ndivyo inavyotakiwa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles