DIAMOND, TUDD WAULA AELA

0
661

NA JESSCA NANGAWE


MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na mwandaaji wa muziki, Tudd Thomas, wote kutoka Tanzania wameshinda tuzo za African Entertainment Legends Awards (AELA) juzi jijini Lagos, Nigeria.

Diamond Platnumz ameshinda tuzo ya kolabo bora ya mwaka 2017 kupitia wimbo wake wa ‘FIRE’ aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria, Tiwa Savage.

Kwa upande wa mtayarishaji, Tuddy Thomas, alinyakua tuzo ya mwandaaji bora wa muziki kwa mwaka 2017 barani Afrika.

Wengine walioshinda tuzo hizo ni Davido kupitia wimbo wake wa Coolest Kid in Afrika kwenye kipengele cha video bora ya mwaka, Run Town, Black coffee na wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here