29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mwakyembe ataka Klabu zisajili vijana

Anna Potinus- Dar es salaam

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka Klabu zote nchini kusajili timu za vijana na iwapo watashindwa kutekeleza agizo hilo hawatoruhusiwa kushiriki kwenye ligi kuu msimu ujao.

Ametoa kauli hiyo leo Juni 15, wakati akizungumza katika harambee ya kuichangia Klabu ya yanga iliyopewa jina la kubwa kuliko ambayo imefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Itakua mwiko tunavyoingia msimu unaokuja kwa timu yoyote ligi kuu isiyo na timu ya vijana kuruhusiwa kushiriki kwenye ligi kuu, hii ni kanuni ninawahakikishia tutaifuata safari hii, tuamue kucheza soka au tucheze michezo mingine ,” amesema.

Aidha amesema kuwa amezungumza na wataalamu kutoka Muungano wa Mashirikisho ya Soka Barani Ulaya (UEFA), na amewaomba kuzisaidia kitaalamu timu za hapa nchini kutengeneza ratiba ya ligi kuu na hata daraja la kwanza.

“Watanzania tuamue kama tunaweza kucheza soka tucheze kama hatuwezi tucheze karata, haiwezekana ukawa na ligi nzuri kwa ratiba kichaa inayokuelekeza leo uko Kagera kesho Mwanza, keshokutwa uko Kagera tena huku ni kuchosha timu na kuongeza gharama,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles