23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wajitokeza harambee ya Yanga, Rostam atoa milioni 200

Anna Potinus – Dar es salaam

Viongozi mbalimbali wamejitokeza katika harambee ya kuchangia klabu ya Yanga SC ambapo wametoa michango yao kwa lengo la kuisaidia klabu hiyo kufikia malengo yake ikiwemo la kufanya usajili msimu ujao.

Harambee hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa Yanga imefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amewakilisha mchango wake wa shilingi milioni 10 ambapo amewataka watu wote kuchangia chochote walichonancho kusaidia klabu hiyo.

“Tutumie fursa ya leo kwa kila mmoja kuchangia chochote alichonacho ili kuwezesha timu yetu kuwa na akiba ya kutosha maana bila Yanga imara tusitegemee mafanikio makubwa huko nje kwenye mashindano ya kimataifa, na mtambue kuwa bila Yanga imara hatuwezi kuwa na Simba Imara na bila Simba imara hauwezi kuwa na Yanga imarapia hivyo nami ninaungana na wanayanga kwa kutoa mchango wangu wa shilingi milioni 10,” amesema.

Akihitimisha hotuba yake Majaliwa ametoa salamu kutoka kwa nfanyabiashara maarufu nchini na mwanachama wa klabu ya Yanga Rostam Aziz ambaye amechangia timu hiyo kiasi cha chilingi milioni 200 na kuahidi kuzikabithi pindi atakapowasili nchini akitokea nchini Marekani.

“Mheshimiwa Rostam Aziz ambaye yuko Marekani ameniambia nitamke mbele yenu kuwa anachangia shilingi milioni 200 na amesema atakaporudi atanijulisha na atakapokuwa anakabidhi ataeleza mchango wake kwa timu ya yanga,” amesema.

Nae rais mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete alihudhuria harambee hiyo na kutoa mchango wake wa shilingi milioni tano ambapo amewataka viongozi wa timu zote nchini kuwekeza kwenye timu za watoto na kuachana na tabia ya kuchukua wachezaji kutoka nje ya nchi.

”Viongozi wekezeni kwenye timu ya watoto kwani msipofanya hivyo mtakuwa na fahari ya kupokea wachezaji kutoka nje, mnachokifanya mnawafundishia wenzenu mnawekeza fedha nyingi kuajiri makocha wanakuja kufundisha wachezaji wa nje halafu siku ya timu ya taifa hawapo,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameahidi kuipatia kabu hiyo eneo kwaajili ya kujenga uwanja kama mchango wake wa kuwasaidia kufikia malengo yao ambapo amesema kuwa timu kubwa kama hizo zinapofanya michezo Mkoani hapo huchangia kukuza uchumi wa nchi.

“Kuanzia jumatatu nitakuwepo ofisini na wataalamu wa ardhi ili mtupatie nyaraka zenu tuwape eneo mjenge uwanja wakati Simba wanaenda Mwagwepande Yanga wanaenda Kigamboni tunakutana uwanja wa Mkapa ,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles