Na Omary Mlekwa, Hai
Abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Arusha kuelekea mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Dar es Salaam na mikoa mingine, wameshindwa kuendelea na safiri kutokana na kujaa yaliyokuwa yakipita Juu ya daraja la mto Biriri.
Maji hayo yametokana na mvua zilizonyesha ukanda wa Mlima wa wilaya ya Siha na kutiririsha maji kupitia mto Lawate, Mto Sanya na kukutana na Mto Biriri.
Daraja hilo lililoko eneo la kwa Wasomali wilayani Hai, limejaa Maji na magogo yaliyotawanywa na maji kutokana mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Kilimanjaro.
Hali hiyo imesababisha abiria kukaa njiani kwa takribani saa nne kusubiri maji yapungue ili waendelee na safari.