30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Musoma aachia ngoma mpya

Na Ramadhan Hassan, Mtanzania Digital

MSANII wa Bongo Fleva, Giraruma Kisheri maarufu kwa jina la Musoma ameachia wimbo mpya unaoitwa  Malalamiko ambao amemshirikisha  Coclyn,  huku akihidi kuendelea kutoa nyimbo zenye ujumbe na zinazowakonga Watanzania.

Musoma ambaye anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwamo ‘Umenichota’  aliomshikirisha staa wa Bongo Star Search, Mesha Mazing, Miss Dom aliomshirikisha One Six na Njoonjoo na Zamu yetu.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Desemba 1,2021, msanii huyo ambaye ni mwalimu wa shule ya Msingi Amani ya Dodoma, amesema wimbo wa Malalamiko umekuja kueleza kwa kina kuhusu usaliti ambao umekuwa ukitokea katika jamii.

Musoma amesema matarajio yake ni kuendelea kutoa nyimbo zenye kuelimisha,kuburudisha na kuonya jamii juu ya mambo mbalimbali huku akisisitiza watanzania wazidi kumuunga mkono.

Katika hatua nyingine, amesema anatarajia  kutoa wimbo uitwao ‘Yatima’ ambapo amedai   atamshikisha msanii mwenye jina kubwa hapa nchini Linex.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles