24.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi Kagera wauwa majambazi

Renatha Kipaka, Biharamulo

JESHI la Polisi Mkoani Kagera limewauwa watu watatu wanaodhaniwa  kuwa ni majambazi  walipokuwa wamejiandaa kwa utekaji wa magari katika eneo la Nyabugombe, Kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo.

Kamanda wa jeashi hilo, Awadhi Jumaa, amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane  ambapo Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa wapo watu wapatao saba wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameonekana katika milima ya Nyabugombe wakiwa wamevaa makoti marefu ndipo Polisi wakaweka mtego ambapo waliwasimamisha kwa ajili ya kuwahoji ndipo  watu hao walianza kujibizana kwa risasi.

“Askari wetu walirushiana risasi na watu hao wapatao saba na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu ambao walifariki wakati wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitli  teule ya Biharamulo huku wengine  walifanikiwa kuroka kabla hawajakamatwa, askali wetu waliendelea kufanya upekuzi ambapo walifanikiwa kukuta silaha moja aina ya AK 47 iliyofutika namba na magazine mbili zikiwa na risasi 51 na kitambulisho kimoja cha Burundi chenye jina la Coyitungiye Venancie mkwilima wa Muyinga Burundi”ameeleza Kamanda.

Kamanda Jumaa amesema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali teule ya Biharamulo kwa uchunguzi wa madakitari .

” Msako mkali bado unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata majambazi wengine waliotoroka ili kukomesha vitendo hivyo vya uhalifu,”amesema Jumaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles