23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Musk ateua bosi mpya Twitter

California, Marekani

Mmiliki wa mtandao wa Twitter, Bilionea Elon Musk amesema kwamba amempata Mtendaji Mkuu mpya wa kuongoza mtandao huo.

Alitangaza habari hizo kwenye mtandao wa kijamii, alioununua mwaka jana kwa $44bn (£35.2bn). Musk hakumtaja Mkuu mpya wa tovuti hiyo lakini alisema “yeye” angeanza baada ya wiki sita, ambapo atakuwa Mwenyekiti Mtendaji na Afisa Mkuu wa teknolojia.

Amekuwa chini ya shinikizo la kutaja mtu mwingine kuongoza kampuni na kuzingatia biashara zake nyingine.

Mwaka jana, baada ya watumiaji wa Twitter kumpigia kura ya kumtaka aachie ngazi katika kura ya maoni mtandaoni, alisema: “Hakuna anayetaka kazi hiyo ambaye anaweza kuiweka Twitter hai,” alisema Musk.

Hata hivyo, ijapokuwa, Musk alikuwa amesema angekabidhi majukumu, haikuwa wazi ni lini au hata ikiwa ingefanyika.

Hisa za Tesla ziliongezeka baada ya tangazo. Hapo awali, Musk alishtumiwa na wenye hisa kwa kuitelekeza Tesla baada ya kuchukua Twitter na kuharibu chapa ya kampuni hiyo ya magari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles