27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kutoa Visa maalum kwa wagonjwa wanaotoka nje

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

MWENYEKITI wa Kamati ya Taifa Utalii wa Matibabu, Profesa Mohamed Janabi ameoimba Serikali kuwapa Visa Maalumu kwa ajili ya wagonjwa wanaotaka kuja kutibiwa nchini na nje ya nchi

Hayo amezungumza Mei 10, jijini Dar es Salaam na Madaktari, Taasisi, Wizara na wadau mbalimbali, wakati wakizindua ripoti na tathimini ya kamati hiyo, Profesa Janabi amesema kuwa kamati hiyo yenye wajumbe 13 imefanya kazi kwa muda wa miaka mitatu bado mwaka mmoja.

“Hawana visa ya tiba maalum kuna wakati mgonjwa anashida ya moyo huwezi mwambia asubiri wiki tatu au mwezi na kuendelea visa zinachelewa kutoka na mgonjwa anahitaji kutibiwa kwa uharaka,”amesema Prof. Janabi

Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kamati hiyo mwaka jana zaidi ya wagonjwa 600 waliotoka nchi za jirani na wana uwezo wa kufundisha nchi hizo.

Amesema lengo la Serikali kupokea watalii milioni tano kutoka nchi mbalimbali lakini hospitali hizo zinatarajia kupata watalii tiba laki tano ifikapo mwaka 2030.

Aidha amesema hospitali zilizopo kwenye watalii tiba ni nne pamoja na hospitali ya Taifa Muhimbili, Moi, Jakaya Kikwete na Ocean Road.

“Asilimia 90 tumepunguza wagonjwa kwenda nje ya nchi, tuna tibu magonjwa figo, moyo, saratani ya damu, kiharusi na uvimbe kichwani na tunatarajia kuzindua mtambo mkubwa juni 1,” amesema Prof. Janabi.

Amesema kuwa kwa mwaka Barani Afrika wanatumia bilioni 4.2 kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

Profesa Janabi amesema asilimia kubwa wagonjwa tunawapeleka India hivyo wana peleka watu kumi kwenda kujifundisha jinsi ya kutoa huduma na watakaa wiki moja nchini humo.

Nae mgeni rasmi Mratibu wa Matibabu Nje ya Nchi kutoka Wizara ya Afya, Dk. Asha Mahita wakati akizindua ripoti hiyo amesema watengeneze imani na uaminifu kwa wagonjwa wanaotoka nje kuja kutibiwa nchini.

Amesema watafanyia kazi yale waliopendekeza pia tiba utalii itaongeza pato la hospitali na pato la Taifa kwa ujumla.

“Kila hospitali iamue inataka kufanya kitu gani? Na Wizara tutatoa muongozo na msiache vitu vikabaki aibu yenu na aibu ya Serikali na kamati ikishindwa itself hela mfukoni,”amesema Dk. Mahita.

Aidha amesema wameweza kuwambia wahusika kujali wagonjwa vizuri na wananchi wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles