24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

EAC yamtaka kiongozi wa DR-Congo kuheshimu mamlaka ya jeshi la kikanda

Kinshasa, DRC

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imemtaka Kiongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuheshimu hatua ya mataifa ya kikanda ya kupeleka vikosi katika jaribio la kuleta utulivu katika maeneo ya mashariki mwa nchi yake.

Siku ya Jumanne, Rais Félix Tshisekedi wa DRC, alishutumu jeshi la Afrika Mashariki kwa kutofanya kazi yake, akionya huenda likaombwa kuondoka nchi humo kufikia Juni.

Pia alishutumu jeshi hilo kwa kushirikiana na waasi wa M23.

Katibu Mkuu wa EAC, Peter Mathuki alisema hajapokea mawasiliano yoyote kuhusiana na malalamiko ya Tshisekedi, akisema masuala yoyote yatakayoibuliwa yatajadiliwa na wakuu wa nchi za EAC.

“Naomba tuheshimu na kuami ni wanachama wa mkutano wa [EAC] kwa sababu najua wana nia ya kutatua suala hili,” Mathuki aliambia NTV ya Uganda siku ya Alhamisi.

Mkuu huyo wa EAC hapo awali aliambia kituo cha redio cha Ufaransa RFI kwamba ukosoaji wa kikosi hicho haukuwa na msingi.

“Kusema kwamba jeshi la kikanda halifanyi lolote, kwa muda mfupi kama huo, si sawa,” alisema, ingawa alikiri kwamba kasi ya kuleta utulivu DR Congo “inaweza isiwe vile tulivyotarajia,” alisema.

Ukosoaji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya jeshi la Afrika Mashariki umekuja siku moja baada ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuidhinisha kupelekwa kwa wanajeshi mashariki mwa nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles