33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MUSEVENI ASAINI SHERIA ITAKAYOMWEKA MADARAKANI HADI 2031

KAMPALA, UGANDA


RAIS Yoweri Museveni amesaini kuwa sheria muswada wenye utata wa Marekebisho ya Katiba No. 2 wa mwaka 2017, yanayoondoa ukomo wa miaka 75 kwa wagombea urais na kuwaongezea wabunge miaka miwili zaidi kuhudumia majimboni.

Uamuzi huo, umemsafishia njia Museveni (75) kuwania urais kwa muhula mwingine wa saba wakati uchaguzi wa rais utakapofanyika mwaka 2021.

Aidha sheria mpya imerudisha ukomo wa mihula miwili ya urais, ambayo iliondolewa wakati wa ujio wa vyama vingi mwaka 2005.

Hata hivyo, kipengele hiki kitaanza kutumika kuanzia uchaguzi mkuu ujao na hivyo Museveni anaweza kutumikia mihula mingine miwili zaidi itakayomweka madarakani hadi 2031.

Hatua ya wabunge kuupitisha muswada huo, inaonekana kama kulipa fadhila baada ya umri wao na maofisa wa Serikali za mitaa kukaa madarakani, kurefushwa kutoka miaka mitano hadi saba, ikimaanisha uchaguzi wa wabunge utafanyika mwaka 2023 badala ya 2021.

Baada ya mjadala wa siku tatu ukipingwa vikali na wabunge wa upinzani, huru na wachache kutoka chama tawala cha NRM, Bunge lilipitisha kile kilichokuja kujulikana kama Muswada wa Ukomo wa Umri.

Wakati wa usomaji wa tatu wa muswada huo, ikiwa hatua ya mwisho kabla ya kuwa sheria, wabunge 315 walipiga kura kuunga mkono, huku 62 wakiukataa na wawili wakijiweka pembeni.

Wakati wananchi wengi wakionekana kutofurahishwa kwa Katiba kurekebishwa mara kwa mara kwa ajili ya mtu mmoja tu; Museveni, wafuasi wake wanadai ni Waganda ndio wanaweza kumwondoa madarakani kwa kura.

Lakini wapinzani wanahisi kuwa uchaguzi haujawahi kuwa huru na hautakuwa huru kwa siku za usoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles